Thursday, June 9, 2011

Mfungwa Aukata Uume Wake ili Awe Mwanamke


Mfungwa mmoja wa kiume wa nchini Marekani ambaye siku zote amekuwa akijihesabu yeye mwenyewe kuwa ni mwanamke amejikata uume wake kwa kiwembe ili kuishinikiza serikali ya Marekani imfanyie operesheni ya kuziondoa sehemu zake nyeti za kiume na kumpandikiza nyeti za kike.
Mfungwa huyo Ophelia De'lonta mwenye umri wa miaka 50, aliamua kuchukua uamuzi huo wa kuukata uume wake kwa kutumia kiwembe na kisha aliifungulia mashtaka serikali ya Marekani kwa kushindwa kumpatia matibabu ya kubadili jinsia yake ili awe mwanamke.

De'lonta ambaye alizaliwa mwanaume akiwa na ugonjwa wa kutamani jinsia tofauti, amefungwa kwenye jela ya wanaume ya Buckingham Correctional Centre na alisema kuwa iwapo hatashinda kesi aliyoifungulia serikali basi ataendelea kujaribu "kukitaka kidude kilichopo kati kati ya miguu yake ambacho ndio dalili pekee ya yeye kuwa mwanaume".

De'lonta alisema kuwa alijaribu kujifanyia mwenyewe operesheni ya kuuondoa uume wake ingawa alikuwa akijua fika kuwa kuukata uume wake kwa kiwembe angeweza kupoteza maisha yake.

Alipokuwa na umri wa miaka 18, De'lonta alihukumiwa kwenda jela miaka 70 kwa makosa ya ujambazi, umiliki wa madawa ya kulevya na silaha.

De'lonta ana matiti makubwa kama mwanamke na aliruhusiwa kuvaa nguo za kike mwaka 2004 baada ya kushinda kesi aliyoifungua mahakamani akitaka apewe homoni za kike za kuongeza ukubwa wa matiti.

De'lonta alisema kuwa aliamua kuukata uume wake baada ya afisa mmoja wa jela kumwita jina lake kama "Bwana De'lonta" wakati yeye alikuwa akipenda aitwe "Bi. De'lonta".

Aliuziba mlango wake kwa makaratasi na kisha alijaribu kuukata uume wake kwa kufuata maelezo aliyoyapata kwenye kitabu cha masuala ya anatomy.

Alipoteza fahamu kufuatia kitendo hicho na alipozinduka alijikuta akifanyiwa operesheni ya kuunganisha uume wake.

No comments:

Post a Comment